Marudio ya Likizo: Kiswahili Kidato cha Kwanza

Jiandae kwa Kidato cha Pili kwa maswali 50 ya kuchagua yenye muda na maswali 20 ya kimuundo, kutoka mada za Kiswahili Kidato cha Kwanza katika mtaala wa TIE.

Jinsi marudio haya yanavyofanya kazi

Bonyeza Anza, kisha chagua jibu. Ukipatia utasikia sauti ya pongezi. Ukikosea utaona jibu sahihi na maelezo. Unaweza pia kubonyeza Angalia jibu bila kupata alama. Una dakika 40, na asilimia yako huonekana mwishoni.

Tanbihi ya Mwalimu: baadhi ya vipengele vya mitihani vilikuwa na majibu yenye utata au makosa ya miongozo (mfano, idadi ya silabi za 'walifundishwa' na mkazo wa 'sanduku'). Vimeandikwa upya hapa ili jibu moja tu liwe sahihi.

Sehemu A: Maswali 50 ya kuchagua

40:00Umejibu 0/50Alama 0

1Mbemba aliwaomba wenzake wamtajie mchakato wa kutuma na kupokea ujumbe kati ya mzungumzaji na msikilizaji. Walipaswa kujibu:

2Kiswahili huwaunganisha Watanzania wa makabila mbalimbali sokoni na shuleni. Hii ni dhima gani ya lugha?

13Katika sentensi 'Mama alikuwa nyumbani', neno 'alikuwa' ni

19Ni sentensi ipi ina mpangilio sahihi wa maneno?

25Neema anauliza kwa nini kamusi ina picha. Jibu bora ni

32Fasihi ni

37Ni seti ipi ina matawi ya sanaa pekee?

Sehemu B: Maswali 20 ya kimuundo

Andika jibu lako kwanza, kisha bonyeza Angalia jibu ulinganishe.

3Amina anataka kamusi lakini wazazi wake wanaona ni upotevu wa fedha. Toa hoja tatu za kuwashawishi.

4Eleza faida tano za picha na michoro katika kamusi.

5Eleza maana ya: lafudhi, lugha ya mazungumzo, fasihi, utamaduni, sarufi.

6Fasili maneno haya: lugha, nomino, tafsida, mawasiliano, kamusi.

12Andika kwa mpangilio sahihi: (a) Mafuta gari limeisha (b) Darasani fimbo alituchapa mwalimu (c) Mdogo mama amekuja yangu jana.

13Tunga sentensi: 'vizuri' kama kielezi na kama kivumishi; 'mama' kama nomino na kama kihisishi.

14Bainisha vitenzi: (a) Mtoto amekwisha oga (b) Yeye hakutaka kunisikiliza (c) Bibi anakula ugali.

16Eleza maana ya kiimbo, kisha eleza lengo la: Kaka analima? / Kaka, lima! / Juma analima kwa bidii!

18Taja vipengele vitano vya fani na vitano vya maudhui. Toa tofauti tatu za fasihi simulizi na andishi.

19Mwalimu Makoye anakataza michezo. Toa hoja tano za kumshawishi aruhusu michezo shuleni.

20Andika barua ya kirafiki kwa mzazi ukimjulisha kuwa utashiriki mashindano ya insha wakati wa likizo.