Darasa la Nne | Kiswahili

Kiswahili Darasa la Nne: Maswali na Majibu

Rudia somo lako likizoni kwa maswali 50 ya chaguo yenye muda na maswali 15 ya kimuundo. Chagua jibu ili ujipime, sikiliza sauti za matokeo na ufuatilie asilimia yako. Maswali ya kimuundo yana majibu ya kubofya.

Maswali 50 ya ChaguoMaswali 15 ya Kimuundo

Jinsi ya Kutumia Ukurasa Huu

Kwenye maswali 50 ya chaguo: bofya jibu unaloona ni sahihi. Ukipatia utasikia sauti ya pongezi na jibu litakuwa kijani. Ukikosea, jibu sahihi na maelezo yataonekana. Muda huanza ukijibu swali la kwanza, na alama na asilimia husasishwa kiotomatiki. Kwenye maswali 15 ya kimuundo, jaribu kwanza kwenye daftari kisha bofya kuona jibu. Mada ni pamoja na sarufi, misamiati, methali, nahau, vitendawili na ufahamu.

Alama za Chaguo: 0 / 50   (0%)
Muda: 00:00

Maswali 50 ya Chaguo (MCQs)

Bofya herufi ya jibu unalochagua. Jibu sahihi hupiga sauti ya pongezi na kuwa kijani. Jibu lisilo sahihi huonyesha jibu sahihi na maelezo. Asilimia ya alama zako huonekana juu, na muhtasari kamili pamoja na muda hutolewa ukimaliza maswali yote 50.

  1. Tulipokuwa tukijisomea aliniambia nikamilishe sentensi hii: “babu na bibi _____ kumwona shangazi kesho.”

    1. Watakwenda
    2. Na
    3. Huenda
    4. Walikwenda
    5. Wanakwenda
  2. Baba yangu alikula wali _____ kijiko.

    1. Kwa
    2. Na
    3. Mwa
    4. Pamoja
    5. Katika
  3. Dereva ni kwa mwendesha vyombo vya nchi kavu, rubani ni kwa mwendesha ndege. Je, nahodha ni kwa?

    1. Vyombo vya majini
    2. Manju
    3. Ni kwa mabaharia
    4. Vyombo vya angani
    5. Treni
  4. Upi ni ukanushi sahihi wa neno “Ataimba”?

    1. Hataimba
    2. Huimba
    3. Ataimba
    4. Hajaimba
    5. Aliimba
  5. Neno lipi ni kisawe cha “zeruzeru”?

    1. Albino
    2. Chotara
    3. Suriama
    4. Muakasti
    5. Mweupe
  6. Yakinisha sentensi: “Elimu haina mwisho.”

    1. Elimu ina mwisho
    2. Elimu si mwisho
    3. Elimu inafika mwisho
    4. Elimu ni mwisho
    5. Elimu haina mwanzo
  7. Neno “mchwa” linaundwa na silabi zipi?

    1. M, chwa
    2. M, c, h, w, a
    3. M, ch, wa
    4. Mchwa
    5. Mch, wa
  8. Jamila anafanya kazi katika maktaba ya taifa. Je, Jamila ni nani?

    1. Mkutubi
    2. Maktabalisti
    3. Mfanyakazi
    4. Mnajimu
    5. Mwandishi
  9. Neno “Kalumanzila” lina silabi ngapi?

    1. Tano
    2. Tatu
    3. Nne
    4. Kumi na moja
    5. Sita
  10. Neno gani lina maana sawa na mwanamke mzee?

    1. Ajuza
    2. Abu
    3. Shaibu
    4. Buda
    5. Bibi
  11. Wingi wa neno “kitoto” ni upi?

    1. Vitoto
    2. Mtoto
    3. Chitoto
    4. Watoto
    5. Vitoto
  12. Neno “msigombanie” lina silabi mwambatano ngapi?

    1. Moja
    2. Mbili
    3. Tatu
    4. Nne
    5. Tano
  13. Wingi wa sentensi “Samaki mkunje angalli mbichi” ni upi?

    1. Samaki wakunje angali wabichi
    2. Masamaki yakunje yangali mabichi
    3. Samaki mkunje wabichi
    4. Samaki wabichi yakunjwe
    5. Samaki wakunjwe
  14. Mtu anayeangua nazi anaitwaje?

    1. Mkwezi
    2. Muanguaji
    3. Mgemaji
    4. Mkunazi
    5. Mchuma
  15. Umoja wa sentensi “Wajuaji wale hawatafanikiwa” ni upi?

    1. Mjuaji huyu hatafanikiwa
    2. Wajuaji hawa hawatafanikiwa
    3. Hatafanikiwa mjuaji
    4. Mjuaji huyu atafanikiwa
    5. Wajuaji wale watafanikiwa
  16. Nahau “kata shauri” ina maana gani?

    1. Amua
    2. Kubaliana
    3. Shirikiana
    4. Kata tamaa
    5. Fikiria
  17. Mtoto wa kwanza katika familia hujulikana kama?

    1. Mziwanda
    2. Kitinda mimba
    3. Kilembwe
    4. Mwanambee
    5. Mwanamume
  18. Nahau “mwaga unga” ina maana gani?

    1. Kufukuzwa kazi
    2. Kuwahi kazini
    3. Kumaliza kazi mapema
    4. Ajiriwa
    5. Kupata kazi
  19. Jibu la kitendawili “Gari moshi relini” ni lipi?

    1. Zipu
    2. Treni
    3. Msitu
    4. Reli
    5. Dereva
  20. Jibu la kitendawili “Liwali amekonda sana lakini hana dawa” ni lipi?

    1. Sindano
    2. Sisimizi
    3. Siafu
    4. Pini
    5. Kalamu
  21. Jibu la kitendawili “Loo! nalipa faini kosa lisijui” ni lipi?

    1. Usingizi
    2. Kutereza
    3. Kujikwaa
    4. Kuanguka
    5. Kosa
  22. Malizia methali: “Asiyekubali kushindwa _____.”

    1. Si msindani
    2. Hawezi
    3. Hathaminiki
    4. Hatashinda
    5. Hafanikiwi
  23. Maige huuza bidhaa kwa bei ya rejareja kwa kuzunguka nazo mtaani. Je Maige ni nani?

    1. Machinga
    2. Dalali
    3. Muuzaji
    4. Mhandisi
    5. Mfanyabiashara
  24. Ni methali gani inasisitiza kuhifadhi chakula kwa matumizi ya baadaye?

    1. Akiba haiozi
    2. Haba na haba hujaza kibaba
    3. Chovya chovya humaliza buyu la asali
    4. Chembe na chembe mkate hua
    5. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu
  25. Wingi wa neno “jiwe” ni upi?

    1. Mawe
    2. Majiwe
    3. Vijiwe
    4. Jiwe
    5. Maji
  26. Neno “adhuhuri” lina silabi ngapi?

    1. Nne
    2. Nane
    3. Sita
    4. Saba
    5. Tano
  27. Kisawe cha neno “adabu” ni kipi?

    1. Heshima
    2. Akili
    3. Utundu
    4. Uvivu
    5. Ujinga
  28. Mwembe, mpera, mchungwa na msufi kwa pamoja hujulikana kama:

    1. Miti
    2. Matunda
    3. Vyakula
    4. Vyombo
    5. Mimea
  29. Gari hili ni la kifahari kwa sababu lina _____ kubwa.

    1. Thamani
    2. Samani
    3. Zamani
    4. Dhamani
    5. Bei
  30. Mama atakula chakula. Sentensi hii ipo katika wakati gani?

    1. Wakati ujao
    2. Wakati uliopo
    3. Wakati uliopita
    4. Hali ya mazoea
    5. Wakati wa sasa
  31. Kipi ni kitendo cha neno “mavuno”?

    1. Vuna
    2. Vuno
    3. Mvunaji
    4. Kivuno
    5. Mavuno
  32. Wingi wa neno “wembe” ni upi?

    1. Nyembe
    2. Viwembe
    3. Mawembe
    4. Kiwembe
    5. Wembe
  33. Neno lipi lina maana sawa na “tamati”?

    1. Mwisho
    2. Mwanzo
    3. Katikati
    4. Utangulizi
    5. Kati
  34. Neno lipi ni tofauti na mengine: mparachichi, mpera, mgahawa, mkaratusi?

    1. Mgahawa
    2. Mkaratusi
    3. Mparachichi
    4. Mpera
    5. Miti
  35. Nahau “tia chumvi” ina maana gani?

    1. Ongeza maneno ya uongo
    2. Ishi miaka mingi
    3. Weka chumvi kwenye chakula
    4. Nong’oneza mtu jambo
    5. Penda mtu
  36. Andika sentensi “Bibi amepika chakula kitamu” katika wakati uliopo.

    1. Bibi anapika chakula kitamu
    2. Bibi alipika chakula kitamu
    3. Bibi hatopika chakula kitamu
    4. Bibi amepikiwa chakula kitamu
    5. Bibi atapika chakula kitamu
  37. Katika familia, mtoto wa mwisho kuzaliwa huitwa?

    1. Kitinda mimba
    2. Mziwanda
    3. Kilembwe
    4. Mwanambee
    5. Mwanamume
  38. Mfano sahihi wa herufi mwambatano ni upi?

    1. Ndw
    2. B
    3. K
    4. T
    5. A
  39. Nahau “alimuuma sikio” ina maana gani?

    1. Alimwambia siri / alimnong’oneza
    2. Alimpiga
    3. Alimuumiza
    4. Alimcheka
    5. Alimlaumu
  40. Jibu la kitendawili “Kila niendako hunifuata” ni lipi?

    1. Kivuli
    2. Kijiko
    3. Kiatu
    4. Kalamu
    5. Gari
  41. Malizia methali: “Hakuna marefu _____.”

    1. Yasiyo na ncha
    2. Yasiyo na mwisho
    3. Yasiyo na mwanzo
    4. Yasiyo na kati
    5. Yasiyo na kitu
  42. Nahau “pata jiko” ina maana gani?

    1. Oa / olewa
    2. Pata chakula
    3. Pata nyumba
    4. Pata kazi
    5. Pata mali
  43. Malizia methali: “Umoja ni nguvu, _____.”

    1. Utengano ni udhaifu
    2. Utengano ni nguvu
    3. Umoja ni udhaifu
    4. Nguvu ni umoja
    5. Udhaifu ni umoja
  44. Malizia methali: “Polepole ndio _____.”

    1. Mwendo
    2. Haraka
    3. Kasi
    4. Nguvu
    5. Upendo
  45. Nahau “amechapa maji” ina maana gani?

    1. Amekufa
    2. Amekwenda
    3. Amelala
    4. Amekimbia
    5. Amepotea
  46. Jibu la kitendawili “Ubwabwa wa mwana mtamu” ni lipi?

    1. Maziwa ya mama
    2. Chakula
    3. Asali
    4. Sukari
    5. Matunda
  47. Siku ya Jumamosi mimi na wadogo _____ tulienda kutembelea fukwe za bahari.

    1. Wangu
    2. Yangu
    3. Zangu
    4. Wetu
    5. Wao
  48. Mafuriko yalitokea ulipofika msimu wa _____ ambapo kulikuwa na mvua nyingi.

    1. Masika
    2. Vuli
    3. Kiangazi
    4. Kipupwe
    5. Kiangazi
  49. Athuman _____ mrefu kuliko wachezaji wote waliopo uwanjani.

    1. Ni
    2. Na
    3. Wote
    4. Kwa
    5. Zaidi
  50. Wingi wa neno “unga” ni upi?

    1. Unga
    2. Miunga
    3. Maunga
    4. Nyunga
    5. Viunga

Matokeo ya Maswali ya Chaguo

0%

Umepata 0 kati ya 50.

Maswali 15 ya Kimuundo

Jaribu kila swali kwenye daftari kwanza, kisha bofya kitufe kuona jibu na kusikia sauti fupi.

  1. Sarufi na misamiati

    1. Ukanushi wa “ataimba” ni upi?
    2. Kisawe cha “zeruzeru” ni nini?
    3. Wingi wa “kitoto” ni upi?
    4. Mtu anayeangua nazi anaitwaje?
    5. Neno “Kalumanzila” lina silabi ngapi?
  2. Nahau

    1. Maana ya “kata shauri”.
    2. Maana ya “mwaga unga”.
    3. Maana ya “tia chumvi”.
    4. Maana ya “alimuuma sikio”.
    5. Maana ya “pata jiko”.
  3. Methali

    1. Malizia: Asiyekubali kushindwa _____.
    2. Malizia: Umoja ni nguvu, _____.
    3. Malizia: Polepole ndio _____.
    4. Malizia: Hakuna marefu _____.
    5. Methali inayohimiza akiba ni ipi?
  4. Vitendawili

    1. Gari moshi relini → ?
    2. Liwali amekonda sana lakini hana dawa → ?
    3. Kila niendako hunifuata → ?
    4. Ubwabwa wa mwana mtamu → ?
    5. Loo! nalipa faini kosa lisijui → ?
  5. Wingi na umoja

    1. Wingi wa “jiwe”.
    2. Wingi wa “wembe”.
    3. Umoja wa “wajuaji wale hawatafanikiwa”.
    4. Wingi wa “samaki mkunje angalli mbichi”.
    5. Wingi wa “mchanga”.
  6. Majina na kazi

    1. Mtu anayefanya kazi maktabani anaitwaje?
    2. Mwendesha vyombo vya majini anaitwaje?
    3. Muuzaji anayezunguka mitaani anaitwaje?
    4. Mwanamke mzee anaitwaje?
    5. Mtoto wa kwanza anaitwaje?
  7. Wakati na vitenzi

    1. “Mama atakula” iko katika wakati gani?
    2. Andika “Bibi amepika” katika wakati uliopo.
    3. Kitendo cha neno “mavuno” ni nini?
    4. Yakinisha: “Elimu haina mwisho”.
    5. Neno “tamati” lina maana gani?
  8. Jaza nafasi (maneno)

    1. Alijiweka mbele ili achaguliwe kuwa _____ wao. (kiongozi)
    2. Tawi lilianza _____ baada ya kutua ndege wengi. (kunepa)
    3. Alipotuamuru tuondoke tulijawa na _____. (hasira)
    4. Hatukuona ndege isipokuwa _____ tu. (mbayuwayu)
    5. Tulipopata _____ wa kuuguliwa kwake tulikwenda kumsalimia. (ujumbe)
  9. Ufahamu – hadithi ya popo

    1. Mgogoro uliotokea uliwahusu kina nani?
    2. “Juhudi ziligonga mwamba” inamaanisha nini?
    3. Neno “kiama” lina maana gani?
    4. Nani alibaki njia panda?
    5. Hadithi hii inahusu nini kwa ufupi?
  10. Ufahamu – Mzee Pango na nyani

    1. Nyani yupi alikuwa mlinzi?
    2. Nyani walivamia shamba la nani?
    3. Mzee Pango alienda wapi?
    4. Nyani wangapi walikuwepo shambani?
    5. Methali “si kila ashibaye ametoa jasho” inamaanisha nini?
  11. Ufahamu – Majuto

    1. Familia ya Majuto inaishi mtaa gani?
    2. Kwa nini Majuto hapendwi na wazazi?
    3. Kwa nini Baraka na Upendo wanapendwa?
    4. “Juhudi zao hazizai matunda” inamaanisha nini?
    5. Neno “pacha” lina maana gani?
  12. Ufahamu – Daudi na nyuki

    1. Daudi alikwenda porini kufanya nini?
    2. Nyuki wana faida gani kwa binadamu?
    3. Wadudu waliomvutia Daudi walikuwa nani?
    4. Nyumba ya nyuki hujulikana kama nini?
    5. Mwanafunzi asipohudhuria shule bila taarifa huitwaje?
  13. Ufahamu – Mzee Mwanga

    1. Familia inaishi kijiji gani?
    2. Nganda hufanya nini Jumamosi?
    3. Kwa nini familia huvuna mazao mengi?
    4. “Humezea mate” inamaanisha nini?
    5. Habari hii inafundisha nini?
  14. Utungaji – panga sentensi

    1. Panga: (i) Baada ya kusubiri basi liliwasili… (ii) Abiria walishuka… (iii) Liliwasili Mwanza… (iv) Nilishuka kwenda kituo… (v) Tulisafiri kwa amani…
    2. Andika mfuatano sahihi wa herufi (mfano A-B-C-D-E).
    3. Toa sentensi ya kwanza katika mtiririko wako.
    4. Toa sentensi ya mwisho katika mtiririko wako.
    5. Kwa nini mtiririko ni muhimu katika utungaji?
  15. Maswali mchanganyiko

    1. Neno “mchwa” linaundwa na silabi zipi?
    2. Dereva ni kwa nchi kavu, nahodha ni kwa _____.
    3. Mtoto wa mwisho anaitwaje?
    4. Herufi mwambatano mfano ni upi?
    5. Neno “adhuhuri” lina silabi ngapi?

Endelea Kujifunza Bure

Umemaliza maswali haya? Pakua programu ya Click Online Academy uendelee kujifunza bure kwa notisi, mitihani na flashcards zaidi.

Pakua kwenye Google Play

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Maswali haya ya Kiswahili Darasa la Nne yanahusu mada gani?

Yanahusu sarufi, misamiati, matumizi ya lugha, methali, nahau, vitendawili, utungaji na ufahamu.

Maswali ya chaguo na alama vinafanyaje kazi?

Bofya jibu unaloona ni sahihi. Jibu sahihi hupiga sauti ya pongezi na kuwa kijani. Jibu lisilo sahihi huonyesha jibu sahihi na maelezo. Muda huanza ukijibu swali la kwanza, alama na asilimia husasishwa papo hapo, na ukimaliza maswali yote 50 utaona asilimia ya mwisho pamoja na muda uliotumia.

Maswali haya ni bure?

Ndiyo. Unaweza kufanya maswali yote 50 ya chaguo na maswali 15 ya kimuundo bila malipo, na kuendelea kujifunza bure kwenye programu ya Click Online Academy.

Maswali haya yametoka wapi?

Mengi yametoka kwenye mitihani ya Kiswahili Darasa la Nne ya nusu muhula, muhula na ya pamoja, na maswali mengine ya marudio yameongezwa kwa mada hizo hizo, pamoja na maelezo ya kukusaidia kujifunza kutokana na makosa.

← Rudi kwenye Kituo cha Marudio ya Vifurushi vya Likizo