Tanzania · Secondary School · Kidato cha 4 / Form 4 · Kiswahili

Form Four Kiswahili Mid-term 1 Exams

Read the full March 2026 Mid-term 1 paper (Mtihani wa Nusu Muhula) below: eleven questions across Sections A, B and C. Write your own answers on paper first. The marking scheme and earlier years are on the Click Online Academy app.

SarufiSemiFasihiUandishi

Choose a Mid-term 1 paper

The March 2026 paper is free to read below. Earlier Mid-term 1 papers are on the Click Online Academy app.

Form Four Kiswahili Mid-term 1 question paper, March 2026

  1. Read each question carefully and write your own answers on paper first.
  2. The marking scheme (muongozo wa usahihishaji) for this paper is available on the Click Online Academy app.
Paper: Form Four Kiswahili Mid-term 1 Examination, March 2026 Time: 2 hours 30 minutes Marks: Section A 16 · Section B 54 · Section C 30

OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA NUSU MUHULA KIDATO CHA NNE · KISWAHILI · Muda saa 2:30 · Machi, 2026

Maelekezo
  1. Karatasi hii ina sehemu A, B, na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A, na B, na maswali mawili (2) kutoka sehemu C ambapo swali la tisa (9) ni la lazima.
  3. Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B alama hamsini na nne (54) na sehemu C alama thelathini (30).
  4. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  5. Vifaa vya mawasiliano na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  6. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 16)

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi

(i) Maneno yafuatayo yana maana zaidi ya moja isipokuwa

  1. Ua
  2. Mbuzi
  3. Kata
  4. Nyau
  5. Paa

(ii) Kipi ni kipengele kinachohusu mjengo wa kazi ya fasihi?

  1. Mtindo
  2. Muundo
  3. Mandhari
  4. Wahusika
  5. Lugha

(iii) Pande mbili zinazohusika katika lugha ya maandishi ni zipi?

  1. Mwandishi na msikilizaji
  2. Msikilizaji na msomaji
  3. Msikilizaji na mzungumzaji
  4. Msomaji na msimuliaji
  5. Msomaji na mwandishi

(iv) Njia ipi hutunza sauti pamoja na vidokezo vyake katika kuhifadhi kazi za fasihi simulizi kati ya hizi?

  1. Maandishi
  2. Mikanda ya filamu
  3. Mitandao
  4. Kinasa sauti
  5. Masimulizi

(v) Kikundi cha maneno kinachoonesha jamii lililotendwa na mtenda katika sentensi hujulikanaje?

  1. Chagizo
  2. Kitenzi
  3. Kivumishi
  4. Shamirisho
  5. Nomino

(vi) Tungo ipi ina kiambishi rejeshi kati ya hizi?

  1. Anaondoka
  2. Ameondoka
  3. Aliondoshwa
  4. Amejiondoa
  5. Ameondokewa

(vii) “Kushindana na mtu aliyekuzidi kwa kila hali si busara.” Methali zifuatazo zinashabihisha kauli hii isipokuwa

  1. Mwenye pesa si mwenzio
  2. Nazi haishindani na jiwe
  3. Chanda chema huvishwa pete
  4. Mwenye nguvu mpishe
  5. Maji yakija kasi yapishe

(viii) “Kiangazi kiliunguza kikaunguza ……… hatimae mwaka elfu moja mia tisa hamsini na sita mvua zikaanza ijapokuwa kwa mazingo.” Usimulizi huu ni aina gani ya hadithi?

  1. Visasili
  2. Vigano
  3. Soga
  4. Ngano
  5. Tarihi

(ix) “Papai limeiva nyumbani lakini nashindwa kulila.” Kauli hii inawakilisha aina gani ya semi?

  1. Methali
  2. Mizungu
  3. Nahau
  4. Vitendawili
  5. Misemo

(x) “Msaada wako umenifaa sana. Asante!” Neno “Asante” ni aina gani ya neno?

  1. Nomino
  2. Kivumishi
  3. Kielezi
  4. Kitenzi
  5. Kihisishi

Jedwali la majibu:

iiiiiiivvviviiviiiixx

2. Oanisha maana ya dhana katika Orodha A na dhana zinazohusika kutoka Orodha B kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi

Orodha AOrodha B
  1. Sehemu ya neno inayotamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti.
  2. Utamkaji wa maneno unaozingatia kanuni za sauti ya lugha.
  3. Nguvu inayotumika kutamka sehemu fulani ya neno.
  4. Vitamkwa vinavyotamkwa na binadamu kwa kutumia viungo vya sauti.
  5. Jinsi mtu anavyotamka maneno ya lugha.
  6. Kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti.
  1. Lafudhi
  2. Matamshi
  3. Kiimbo
  4. Mkazo
  5. Silabi
  6. Lugha
  7. Sauti

Jedwali la majibu:

iiiiiiivvvi

SEHEMU B (Alama 54)

3. Tumia kiambishi “KA” kuonesha matukio 10

(Andika sentensi 10 zinazotumia kiambishi “-ka-” kuonyesha mfululizo wa matukio.)

4. Yapange maneno yafuatayo kama yanavyoonekana katika kamusi kisha eleza maana ya kila neno kwa kutoa mfano mmoja wa sentensi

FalsafaAjuzaBariziFanusiAnuwaiGhaibuBarubaruGoigoiKindaKinanda

5. (a) Katika kila sentensi, andika neno moja lenye maana sawa na maelezo ya sentensi husika

  1. Mtu anaye chunguza uhalifu
  2. Ng’ombe dume aliyehasiwa
  3. Chombo cha usafiri kinachopita juu ya vyuma
  4. Mti unaozaa matunda yanayotengeneza kinywaji cha kahawa
  5. Sehemu ndogo ya nchi iliyochongoka na kuzungukwa na bahari katika sehemu zake tatu

(b) “Mofimu huru zina hadhi ya neno.” Fafanua usemi huu kwa kutumia sentensi nane (8) tofauti.

6. Toa maana tano tofauti za neno “kibao” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana uliyotoa.

7. Tunga tungo zenye vipashio vifuatavyo

  1. Nomino + kishazi tegemezi + Prediketa + Shamirisho
  2. Kiimakapa + Prediketa + Chagizo
  3. Kirai nomino + Kishazi huru + Kishazi tegemezi
  4. Nomino + Kitenzi + Kielezi

8. Jifanye wewe ni Gulamali Banji anayeishi mtaa wa Tandamti Gerezani Kariakoo na unataka kuuza gari yako aina ya CARINA. Andika Tangazo kwenye gazeti la Mwananchi.

SEHEMU C (Alama 30)

Jibu maswali mawili (2). Swali la 9 ni la lazima.

9. “Fasihi ni nyenzo muhimu katika kutoa mafunzo kwa jamii.” Thibitisha kauli hii kwa kutumia diwani mbili ulizosoma.

10. “Mapenzi ya dhati huleta faraja miongoni mwa wanajamii.” Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila riwaya kati ya riwaya mbili ulizosoma.

11. Kwa kutoa hoja mbili na mifano eleza namna jina la kitabu linavyosadifu yaliyomo katika tamthiliya mbili ulizosoma.

Orodha ya Vitabu

Ushairi

  • Wasakatonge – M.S. Khatibu (DUP)
  • Malenga Wapya – TAKILUKI (DUP)
  • Mashairi ya Cheka Cheka – T.A. Mvungi (EPD. LTD)

Riwaya

  • Takadini – Ben J. Harson (M.A.)
  • Watoto wa Mama N’tilie – E. Mbogo (H.P.)
  • Joka la Mdimu – A.J. Safari

Tamthiliya

  • Orodha – Steve Reynolds (M.A.)
  • Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe – E. Semzaba
  • Kilio Chetu – Medical Aid Foundation

Get the marking scheme and more Mid-term 1 papers on the app

Unlock the marking scheme for this paper, plus 2025, 2024, 2023 and earlier Kiswahili Mid-term 1 papers, with terminal, regional mock and NECTA review papers.

Download on Google Play

Continue with Form Four Kiswahili exams

Next in the exam sequence

Start the year here. After Mid-term 1, move on to the terminal exams, and use the topical exams and online tests to fix weak topics.

Or go back to all Form Four Kiswahili exams, all Form 4 exams or all secondary exams.

Other Form Four Mid-term 1 exams

Practise more subjects

Kiswahili for other classes

Continue on the Click Online Academy app

Unlock every Form 4 Kiswahili paper, topical exams, regional mock papers and NECTA review papers, with progress tracking and offline downloads.

Get the Kiswahili exams on Google Play Back to all secondary exams

Frequently asked questions

Is the Form Four Kiswahili Mid-term 1 2026 paper free?

Yes. The full March 2026 question paper is free to read on this page. The marking scheme and earlier years are on the Click Online Academy app.

What does the Form Four Kiswahili mid-term paper cover?

The March 2026 paper has eleven questions. Section A has ten multiple-choice items and a matching item on language and literature, Section B has short-answer questions on grammar, vocabulary and writing (including sentences with the -ka- tense marker, dictionary order, word meanings and a newspaper advertisement), and Section C asks for essays on the set books for poetry, novels and plays.

Where can I find other Kiswahili exam types?

Online MCQ tests, topical papers, terminal, pre-national, regional mock and NECTA review papers are linked from the exam sequence bar on this page and available in full on the app.