Form One Selection 2027
Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2027
Kiungo rasmi cha TAMISEMI, jinsi ya kuangalia jina la mwanafunzi na hatua zinazofuata.
ANGALIA WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2027 – INAKUJA HIVI KARIBUNI
Orodha ya waliochaguliwa inatolewa na TAMISEMI pekee. Click Online Academy haihifadhi wala kubadili orodha hiyo. / The selection list is published only by TAMISEMI.
Matokeo ya Darasa la Saba 2026 yametoka. Angalia matokeo ya Darasa la Saba 2026 hapa.
Form One Selection 2027 ni nini?
Baada ya matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba (PSLE), TAMISEMI hupanga wanafunzi waliofaulu kujiunga na shule za sekondari za serikali kwa Kidato cha Kwanza. Tangazo hilo ndilo huitwa Form One Selection au Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza.
Mwaka uliopita, TAMISEMI ilitangaza uchaguzi mapema Desemba 2025. Tarehe ya mwaka huu bado haijathibitishwa; tutasasisha ukurasa huu mara tu tangazo rasmi litakapotoka.
Jinsi ya kuangalia Form One Selection 2027
- Bofya kitufe cha ANGALIA WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2027 hapo juu (kitafanya kazi tangazo likishatoka).
- Katika tovuti rasmi ya uchaguzi ya TAMISEMI, chagua First Selection (Uchaguzi wa Kwanza).
- Chagua mkoa ambako mwanafunzi alisoma shule ya msingi (si mkoa atakakosoma sekondari).
- Chagua halmashauri na kisha shule ya msingi.
- Tafuta jina la mwanafunzi kwenye orodha, kisha uhifadhi au upige picha ya ukurasa.
Majina ya menyu kwenye tovuti ya TAMISEMI yanaweza kubadilika. Tovuti ikiwa na watu wengi, jaribu tena baada ya dakika chache.
Mikoa (chagua mkoa wa shule ya msingi)
- Arusha
- Dar es Salaam
- Dodoma
- Geita
- Iringa
- Kagera
- Katavi
- Kigoma
- Kilimanjaro
- Lindi
- Manyara
- Mara
- Mbeya
- Morogoro
- Mtwara
- Mwanza
- Njombe
- Pwani
- Rukwa
- Ruvuma
- Shinyanga
- Simiyu
- Singida
- Songwe
- Tabora
- Tanga
Nini cha kufanya baada ya kuchaguliwa?
Angalia shule aliyopangiwa mwanafunzi, kisha fuata maelekezo ya kujiunga (joining instructions) kutoka shule na mamlaka husika. Wakati huo huo, mwandae mtoto kwa Kidato cha Kwanza:
Walimu: Schemes of Work 2027
Mwaka mpya wa masomo unakaribia. Pata schemes of work kamili za 2027 kwa somo na darasa lako.
Chat On WhatsApp for 2027 Schemes Angalia schemes of work
Maswali yanayoulizwa mara nyingi (FAQ)
Form One Selection 2027 itatangazwa lini?
Tarehe rasmi hutangazwa na TAMISEMI, na bado haijathibitishwa kwa mwaka huu. Uchaguzi wa Kidato cha Kwanza ulitangazwa Desemba 2024 na tena mapema Desemba 2025. Ukurasa huu utasasishwa mara tu tangazo litakapotoka.
Ninaangaliaje majina ya waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2027?
Fungua tovuti rasmi ya uchaguzi ya TAMISEMI kupitia kitufe cha ukurasa huu, chagua mkoa ambao mwanafunzi alisoma shule ya msingi, kisha halmashauri na shule, na utafute jina la mwanafunzi.
Ni taarifa gani ninahitaji ili kuangalia uchaguzi?
Jina la mwanafunzi, shule ya msingi alikosoma, halmashauri na mkoa. Namba ya mtahiniwa ya PSLE pia husaidia kutambua jina sahihi.
Je, wanafunzi wote waliofaulu Darasa la Saba huchaguliwa?
Kwa mwaka uliopita, TAMISEMI ilieleza kuwa wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa Darasa la Saba walipangiwa shule. Kwa mwaka huu, fuata tangazo rasmi la TAMISEMI.
Je, Click Online Academy inatoa orodha ya waliochaguliwa?
Hapana. Orodha rasmi inatolewa na TAMISEMI pekee. Sisi tunakuelekeza kwenye chanzo rasmi, tunakupa maelekezo na rasilimali za kujiandaa na Kidato cha Kwanza.
Nitapataje taarifa mara selection inapotoka?
Fuatilia WhatsApp Channel ya Click Online Academy au rudi kwenye ukurasa huu. Tunaweka kiungo rasmi mara tu kinapopatikana.
Habari zinazohusiana
Matokeo ya Darasa la Saba 2026
Syllabus na Vitabu vya TIE
Habari zote »