Vitabu vya TIE: Sekondari (Kidato cha 1-6)
TIE Books for Secondary School Form 1-6
Fika kwenye maktaba rasmi ya mtandaoni ya TIE kupata vitabu vya masomo yako.
FUNGUA TIE ONLINE LIBRARY TOVUTI RASMI YA TIE
Vitabu vya TIE vya sekondari
TIE Online Library inakusanya vitabu vya kiada vya Kidato cha 1 hadi 6 vilivyoandaliwa kulingana na mtaala mpya. Chagua ngazi (Ordinary au Advanced), kisha kidato na somo.
Kwa maandalizi ya mitihani, tumia pia notes zetu za sekondari na mitihani ya zamani ya NECTA.
Jinsi ya kuipata / How to get it
- Bofya kitufe cha FUNGUA TIE ONLINE LIBRARY hapo juu (ol.tie.go.tz).
- Unaweza kuombwa kujisajili au kuingia (sign in). Fuata maelekezo ya TIE kwenye ukurasa huo.
- Chagua ngazi ya elimu: Sekondari ya kawaida (Form 1-4) au Advanced (Form 5-6).
- Chagua kategoria (kwa mfano Vitabu vya TIE), kisha chagua darasa au kidato na somo.
- Soma kitabu mtandaoni au kwa kutumia njia ambazo TIE inaruhusu.
Upatikanaji wa vitabu na masharti ya kuingia yanawekwa na TIE na yanaweza kubadilika.
Rasilimali za Click Online Academy
Maswali yanayoulizwa mara nyingi (FAQ)
Wapi naweza kupata vitabu vya TIE vya Kidato cha 1-6?
Kwenye TIE Online Library (ol.tie.go.tz) au kupitia tovuti ya TIE. Tumia vitufe vya ukurasa huu.
Vitabu vya mtaala mpya vinapatikana kwa masomo gani?
TIE inaendelea kuchapisha vitabu kwa masomo mbalimbali. Chagua kidato na somo ndani ya maktaba kuona vilivyopo.
Je, ni lazima kujisajili?
Maktaba inaweza kukuomba kujisajili au kuingia. Masharti hayo yanawekwa na TIE.